Tuesday, February 3, 2009

mambo ya mtandao

Hallow,
Leo ikiwa ni siku ya pili katika warsha nimejifunza mengi moja ikiwa ni journalism of the age of Internet.

Katika mada hii imenifundisha umuhimu wa mwandishi wa habari katika kutumia mtandao(Internet)hasa katika kazi zake za kila siku.

Asilimia kubwa ya waandishi wa habari nchini bado hawatumii mtandao ipasavyo katika kuandika habari yawezekana ni kwa sababu ya gharama au kutofahamu kutumia mtandao.

Changamoto kubwa iliyopo ni waandishi wa habari kutumia mtandao kama ambavyo nchi za magharibi zimekuwa zikitumia mtandao katika mausuala ya habari ambayo inaweza kukurahisishia kazi.

Mtandao ni moja ya kitu ambacho kinaweza kukupatia habari kwa haraka tofauti na kusubiri magazeti ama njia nyingine ya mawasiliano.

Kwa miaka mingi Tanzania tumekuwa tukitumia magazeti kufikisha ujumbe ama habari kitu ambacho kimekuwa kikisababisha watanzania wengi kukosa habari muhimu.

Lakini Tangu kuingia kwa vyombo vya habari kama radio na Televisheni imesaidia kwa kiasi kikubwa watanzania wengi kupata habari lakini bado takwimu zinaonyesha kuwa watanzania wengi hawatumii mtandao ipasavyo(internet) na hasa ukizingati asilimia kubwa ya magazeti yamekuwa na website kwa ajili ya kuweka habari zilizo gazetini.

Sina hakika kwa mwenendo huu tunaokwenda nao katika kipindi cha miaka 10 ijayo kama kutakuwa na mwamko wa watanzania kutumia mtandao ,labda linalochangia kubwa ni zaidi asilimia 70 ya watanzani hawana umeme je mtandao wataupata wapi???????

Hii ni changamoto kubwa kwa serikali lakini kwa wadau ambao ni wapenda maendeleo hasa katika dunia hii ya sayansi ya Teknolojia…

No comments:

Post a Comment